Watoto Wa Kambo Wa Regina Daniels Ni Wa Rembo Sana!

Watoto Wa Kambo Wa Regina Daniels Ni Wa Rembo Sana!

Picha za watoto wa kambo wa mwigizaji mashuhuri Regina Daniels zimeibuka kwenye mitandao.

Mwigizaji wa Nollywood na aliye maarufu sana kwa mtandao, Regina Daniels anaonekana kuikumbatia jukumu yake kama mama wa kambo. Maendeleo haya yametendeka baada ya ndoa yao na mwanabiashara bilionea na mmoja wa National Assembly. Kutoka siku hiyo, picha za watoto wa kambo wa Regina Daniels zimejaa kwenye mtandao. Hivi majuzi, picha za mwigizaji huyu na watoto wake kutoka kwa mama mwingine zimeonekana kwenye mtandao.

Habari za maisha ya mapenzi ya mwigizaji huyu na bilionea wake zilianza kuibuka baada ya kuanza kuonyesha watu vitu vya dhamani alivyo miliki. Kulingana na ripoti, bwanake alimnunulia chochote alichotaka, magari ya aina zote. Kwa picha za hivi karibuni alionyesha watu watoto wake wa kambo kwenye Instagram.

Tizama Picha Hizi za Instagram za Watoto wa Kambo wa Regina Daniels

Mwigizaji huyu alikuwa anawafurahisha watoto wake wa kambo walio onekana kupendezwa sana naye. Inasemekana kuwa watoto hawa ni wa bibi anaye toka Morocco wa bilionea huyu.

www.instagram.com/p/B12K_VxjsCE/?utm_source=ig_web_copy_link

Hivi majuzi, mume aliye bilionea alipata tuzo la kumpongeza. Ilitoka Federal University of Petroleum Resources Effurun (FUPRE) huko Delta State. Regina Daniels na watoto wake wa kambo pia walikuweko. Mwigizaji huyu alionekana akifurahia kuwa na watoto wake wa kambo.

www.instagram.com/p/B0oA5MMj5XX/?utm_source=ig_web_copy_link

Inaonekana kana kwamba ulezi umemkubali mwigizaji mashuhuri wetu. Wazazi wengi wa kambo hutatizika kutengeneza familia zinazo sikizana. Na watoto wengi wa kambo wana wakati mgumu kubadilika na kukubali kuwa wazazi wao wana wapenzi wapya. Ni wakati mgumu sana kwao. Jambo unalo paswa kujua ni jinsi ya kusikizana na watoto. Tazama vidokezo tunavyo orodhesha hapa chini.

Jinsi ya kusikizana na watoto wako wa kambo

watoto wa kambo wa regina daniels

Mwache mtoto aongoze

Hakikisha kuwa una heshimu mwendo wa mtoto wako wa kambo. Huenda ikawachukua muda kutaka kukujua. Kwa baadhi ya watoto, huenda ikachukua muda mrefu. Jaribu kuto walaumu. Kuwa mvumilivu na mtulivu.

Iwapo uhusiano wa hapo awali kati ya wazazi wao uliisha kwa talaka, fahamu kwamba watoto hao wanahitaji muda wa kuzoea kilicho tendeka. Uhusiano wako na mzazi wao ni ushuhuda kuwa wazazi wao hawatawahi rudiana. Na huenda kukawatatiza watoto. Wape muda na uwaelewe.

Jaribu matembezi peke yako

Baada yako na mtoto wako wa kambo kujuana kwa muda, unaweza pendekeza matembezi, ya wawili wenu. Huenda jambo hili lika kukwaza kidogo lakini linawezekana.

Chagua jambo ambalo hamlazimishwi kuongea kila wakati. Unaweza chagua mojawapo ya michezo ambayo mtoto wako anapendelea. Iwapo hapendi michezo, unaweza mpeleka akaone sinema.

Unga mkono anacho taka

Hii ni muhimu sana. Baadhi ya njia unazo weza kufanya hivi ni kwa kuwasaidia kufanya kazi yao ya ziada. Hakikisha kuwa maneno yako yana himiza wakati wote. Pia unaweza fanya kitu ambacho wanafurahia kufanya. Kama vile kusoma, michezo, muziki ama vitu vingine na uone iwapo wangependa ujiunge nao.

Omba maoni kutoka kwa watoto wa kambo wa Regina Daniels: Panga na mpenzi wako

Jadiliana na mchumba wako aina ya uhusiano ambao ungependa kuwa nao na watoto wako wa kambo. Anapaswa kuhisi huru kusimama kando na kuwacha uhusiano wenu na watoto ukue kwa njia ya asili.

Kuwa rafiki yao

Ni sawa iwapo hauwapendi watoto wako wa kambo mapema- kuwa na hisia huchukua muda, kwako na pia kwao. Kuwa rafiki mnapo anza ni sawa.

Pulse NG

Soma pia: How to Bond With Your Stepchildren And Build A Great Blended Family

 

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha, kisha yakatafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio