Kampuni Za Wafanyakazi Wa Nyumba Karibu Nami

Kampuni Za Wafanyakazi Wa Nyumba Karibu Nami

Kila mtu ameskia hadithi za wafanya kazi walio potea na watoto baada ya kuwachwa wawatunze, ama wakahusika kwa matendo haramu. Wazazi huwa na woga wanapo fikiria kuhusu kuwa ajiri wafanya kazi. Kama wanawake wengi wa Nigeria wanavyo sema, watu wanao ajiriwa wana faida nyingi hata na habari hasi zikiwa kila mahali. Hii ndiyo sababu kwa nini wamama wengi hutafuta wafanyakazi wa nyumba karibu nami kila mara kwenye mtandao.

Ukweli ni kuwa kuna mamilioni ya wafanyakazi wa nyumba wazuri na walio na vyeti na utu na roho njema ya kuwatunza na kuwalinda watoto.

Kutafuta na kuajiri mfanyakazi wa nyumba sio jambo rahisi. Kuna kampuni nyingi za wafanyakazi wa nyumba, ila baadhi ya kampuni hizi zimepatikana kuwa na wafanyakazi wasio wa kweli.

 Vidokezo vya kuangalia unapotafuta mojawapo ya kampuni za wafanyakazi wa nyumba karibu nami 

1.  Omba ushauri kutoka kwa wana familia na marafiki unao waamini

Inapofika wakati wa kutafuta kampuni zinazo ajiri wafanya kazi wa nyumba, hatua ya kwanza ni kuuliza marafiki na jamii unao waamini.

Katika kazi ya kuwalea watoto, familia nyingi zimekumbana na wafanyakazi wote wazuri na wabaya. Kujaribu kuomba ushauri kutoka kwa walio yapitia kutakusaidia kuamua kampuni utakazo chagua na unazo paswa kukaa mbali zaidi nazo.

2.  Hakikisha unatumia kampuni zinazo julikana

Unapo wasiliana na kampuni yoyote ya wafanya kazi wa nyumba, jaribu kujua wamekuwa kwa tasnia hii kwa muda upi? Iwapo wamekuwa kwa kazi hii kwa muda mrefu, wana aminika kwa sababu kuna baadhi ya makosa kwenye biashara hii ambayo watakuwa wanajaribu kuepuka.

3.  Chagua kampuni iliyo sajili

Kama kampuni zingine rasmi, biashara ya wafanya kazi wa nyumba ina dhibitiwa kama mashirika mengine yanayo julikana na serikali. Utafanya vyema kuangalia iwapo kampuni uliyo chagua ime sajiliwa kuwa ajiri kazi wafanya kazi za nyumbani. Fanya utafiti mwingi uwezavyo.

Majukumu ya mfanya kazi wa nyumba

Unapo fanya utafiti kwenye mtandao kwa kampuni bora zaidi zilizo na 'wafanya kazi wa nyumba karibu nami' unapaswa kujua kuhusu majukumu yake. Baadhi ya wazazi hufanya kosa la kumwajiri mtu kazi bila ya kutaja majukumu wanayo tarajia kutoka kwa wafanya kazi wao.

Kwa watu wengi, wafanya kazi wa nyumba wana weza fanya kitu chochote wanapo kuwa nyumbani. Ila mfanya kazi aliye na vyeti ni mtu aliye na uzoefu na aliye pata mafunzo ya kuwatunza watoto nyumbani. Wana huduma nyingi kama vile kusafisha, kusomesha, kuegemeza watoto kitabia na hisia na kuhakikisha wako salama na kadhalika.

Majukumu ya wafanya kazi wa nyumbani ni kama vile

 • Kuosha nyumba
 • Kusafisha
 • Kuvalisha
 • Kuwabadilisha watoto nguo 
 • Kutengeneza chakula
 • Kununua vitu vya nyumba
 • Kuwapeleka watoto shuleni na kuwachukua
 • Baadhi ya wakati kufanya kazi za ziada na watoto(ila sio wakati wote)wafanya kazi wa nyumba karibu nami

Tabia muhimu unazo paswa kuangalia unapo mwajiri mtu kukuchungia watoto wako

Unapo mtafuta mtu wa kukuchungia watoto, hakikisha kuwa, unatafuta mtu aliye na ujuzi na maarifa katika mambo yafuatayo ya utunzaji wa watoto na ulezi.

 • Uhusiano na wanarika na ndugu zake
 • Kumfunza mtoto kutembe
 • Mafunzo ya maendelezo kama vile mafunzo ya kulala, kutembea na hata kuenda msalani na kadhalika
 • Kusoma na kuandika
 • Maendeleo ya lugha na mazungumzo
 • Michezo bunifu

 

Kumbukumbu: Barnet.gov.uk

Soma pia: The best and most popular schools in Lekki

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio