Tofauti Kati Ya Wazazi Wa Afrika Na Umarekani Na Mbinu Zao Za Ulezi

Tofauti Kati Ya Wazazi Wa Afrika Na Umarekani Na Mbinu Zao Za Ulezi

Mbinu tofauti ambazo wazazi kutoka Afrika wanatumia ambazo ni tofauti na za wale kutoka Umarekani.

Mzazi ni mtu aliye twika jukumu kuu la kuwalinda na walea watoto ama mtoto anaye barikiwa naye. Mbali na hilo, ni kazi yake kuhakikisha kuwa mtoto anakua kwa njia ipasavyo na kupata mahitaji yote maishani. Njia za ulezi zimebadilika ikilinganishwa na siku za hapo awali kwani kuna mengi yanayo zidi kuibuka. Kuna mengi yaliyo semwa kuhusu wazazi wa ki Afrika na mbinu zao za ulezi zilizo tofauti sana na za watu wa ugenini. Makala haya yana angazia tofauti kati ya wazazi wa Afrika na Umarekani. Na kudhibitisha yaliyo ya kweli na yasiyo ya kweli.

tofauti kati ya ulezi wa kiafrika na umarekani

Tofauti Kati Ya Wazazi Wa Afrika Na Umarekani

Utamaduni

Wazazi wa ki Afrika wana fuata utamaduni sana na wengi wao wafuata njia za ulezi ambazo wazazi wao walitumia. Pia wengi wao hawako wazi kutumia njia mpya za ulezi. Utamaduni una piga marufuku kuwa na mazungumzo wazi ya mada tofauti. Kwa tamaduni za Ki Afrika, sio jambo la kawaida kupata wazazi wanazungumza kwa uwazi na watoto wao kuhusu mapenzi na kufanya ngono. Ni vyema kwa wazazi kuwalinda, kuwaongoza na kuwaongelesha watoto wao kuhusu ngono. Kwa njia hii unahakikisha kuwa watoto wako wanapata ujumbe ulio kweli ikilinganishwa na kupata ujumbe kuhusu ngono kutoka kwa wanarika wao. Huenda wakapata ujumbe usio wa kweli na ukasababisha wapate hasara maishani. Utumizi wa kondomu unapaswa kuwa mada kuu kati ya wazazi na watoto wao. Ila, ni vigumu kwa wazazi kuongea bayana kuhusu mambo haya, kwani wana amini kuwa watoto watapotoka zaidi. Ukweli ni kuwa watoto huwa na maisha hai ya ngono kutoka wanapokuwa umri wa miaka minane ama kumi. Kwa hivyo ni vyema kwa wazazi kuanza mazungumzo haya na watoto wao wanapokuwa wachanga ili wakue na ujumbe unaofaa na ulio kweli. Kuwaficha ili wasipotoke kutafanya wakose mwongozo unaofaa na iwapo wata jiingiza katika matendo haya, hawatajua jinsi ya kujikinga. Ni jambo la busara kwa wazazi wa ki Afrika kufahamu kuwa mambo yamebadilika na watoto wanajua mambo mengi. Hauwalindi kwa kuwaficha ila unawalinda kwa kuwapa ujuzi kuhusu kujikinga.

Tofauti Kati Ya Wazazi Wa Afrika Na Umarekani Na Mbinu Zao Za Ulezi

Ikilinganishwa na wazazi wa Umarekani ambao hawafuati tamaduni na mbinu zao za ulezi ni mpya. Mazungumzo yao sio fiche na hakuna kitu wanacho kificha kwa watoto wao. Kwa njia hii, watoto huwa na urafiki wa karibu na watoto wao na wanapo tatizika wanajua kuwa wazazi wao watawasaidia wanapo kwama. Hili ni jambo ambalo wazazi wa kiafrika wanapaswa kufuata ili kuwa na urafiki wa karibu na watoto wao na kuwa na mazungumzo wazi.

Ulezi wa urafiki na ulezi amurisha

Kwa wakati mwingi, unapata kuwa wazazi wa Afrika wana fuata mbinu ya ulezi ya kuamurisha ikilinganishwa na mbinu ya ulezi ya wazazi wa Umarekani ambao ni walezi marafiki. Inajulikana kuwa wazazi wa ki Afrika hawapendi kuwasikiza watoto wao, ila wanacho sema ndicho kinacho paswa kufuatwa bila kubishana ama kupeana maoni yako. Watoto wanawaogopa wazazi wao ambalo halipaswi kuwa. Mzazi anapaswa kuwa rafiki na watoto wake na kuwasikiliza. Kwa njia hii, utapata maoni zaidi na kujua mahali ambapo wanapaswa kurekebisha ama vitu ambavyo watoto wao wangependa. Kimasomo, wanafunzi ambao wana wazazi marafiki, wanafuzu masomoni mwao kwani wanaweza kujadili vitu tofauti na wazazi wao. Wazazi wanao wasikiliza na kuwashauri watoto wao wana wapatia ujasiri na ushupavu zaidi. Mtoto mwenye ujasiri anafuzu katika masomo yake na mambo mengine anayo yafanya.

tofauti kati ya wazazi wa ki afrika na wa Umarekani

Kwa wazazi wa Umarekani, mambo ni tofauti kwani ni marafiki na watoto wao na wana sikiza kwa umakini wanacho sema. Uhusiano huu ni muhimu sana kati ya wazazi na watoto wao na inawasaidia wote wawili. Watoto wanapo kumbwa na matatizo yoyote, wanajua kuwa wanapaswa kuwapigia wazazi wao ili kupata ushauri.

Kuna mengi sana ambayo wazazi kutoka Afrika wanapaswa kuiga kutoka kwa wazazi wa Umarekani ili wawe na uhusiano bora zaidi na wanao na kuhakikisha kuwa wana maisha bora.

Kumbukumbu: Standard media

Written by

Risper Nyakio