Tabia Za Vijana: Kuwalea Watoto

Tabia Za Vijana: Kuwalea Watoto

Miaka ya ujana ndiyo miaka inayo umba maisha ya mtu. Katika kujua tabia za vijana, ni muhimu kukumbuka kuwa hakuna vijana wawili walio sawa. Walakini, vijana wote hupitia mabadiliko ya kifizikia na homoni ambazo zinaweza wa-umba kuwa watu wazima ambao watakuwa kwenye siku zao za usoni.

Sababu kwa nini miaka ya ujana ni muhimu katika ukuaji na maendeleo

Vijana bila shaka wana nishati, wanataka kujua zaid, hawana uwoga na wanataka kujaribu mambo mapya. Wanakua katika hatua hii na hawana uwoga kujaribu mipaka na kudhibitisha uhuru wao. Kulea kijana kutakuja na changamoto zake. Ili kufanya kazi ya kufuzu ya kuwaongoza vijana kwenye uzima wao, utapaswa kuelewa tabia za vijana.

Baadhi ya Tabia Muhimu za Vijana:

tabia za vijana

Vijana wanapitia wakati wa ukuaji

Tunapo sema ukuaji, tuna maanisha kuwa vijana wanakua kifizikia, hisia na kijamii. Ukuaji huu pia huwafanya watake kujua zaidi kuhusu mapenzi na huenda hata wakaanza majaribio. Watu wachanga kati ya umri wa miaka 13-18 hupitia mabadiliko mengi ya homoni wakiji tayarisha kuwa watu wazima.

Wasichana hutoa estrogen zaidi katika kipindi hiki na huenda wakapitia nyakati ya mabadiliko ya utu uzima. Mabadiliko yanayo kusudiwa kwenye wasichana ni kama vile kuanza hedhi, kukua nywele katika sehemu nyeti, matiti na kuwa warefu zaidi.

Wavulana katika rika hili huanza kutoa testosterone zaidi. Pia wanakua nywele za uso na mwili. Ukuaji katika wavulana huwa mkuu zaidi ikilinganishwa na wasichana. Wavulana wanaweza kua inchi 20 zaidi na kuwa na uzito zaidi.

Kijamii, vijana hupenda kuwa na marafiki wao wakati mwingi. Katika hatua hii ya maisha yao, pia wanakua kihisia na kifizikia. Sio jambo lisilo la kawaida wakaanza kufanya majaribio ya kufanya mapenzi pia.

tabia za vijana

Vijana hawana uoga kupita mipaka

Watu wengi huamini kuwa tabia za vijana kama vile kuwapinga watu na kuto watii, ila kuna sababu kwa nini kijana wako anafanya jinsi anavyo. Walakini, sio vijana wote huwapinga wazazi. Wanao kuwa wapingamizi sio kwa sababu wanataka kujaribu uvumilivu wako.

Kulingana na BBC Science, kijana wako hafanyi anavyo fanya kwa sababu yeye ni mbaya. Wana kua na wanajaribu kuwa na utu wa kibinafsi. Tatizo ni kuwa baadhi ya uamuzi wetu huenda ukakosa kuwa mzuri kulingana na watu wazima.

Iwapo inaonekana kuwa vijana wako wana bishana nawe mara kwa mara, unapaswa kukumbuka kuwa hisia zao huenda zikabadilika kwa sababu homoni mwilini mwao zina badilika pia. Ukikumbuka tabia hizi za vijana, itakuwa rahisi kwako kutangamana na watu wa rika hili.

Vijana hupitia wakati wa ukuaji wa mawazo

Vijana wengi watakuambia bila fiche kuwa wao sio watoto tena. Kwa njia moja, wana ukweli. Kulingana na makala haya yaliyo chapishwa kwenye Healthy Place for Mental Health, watu wachanga kwenye umri wa miaka 11-18 wana uwezo wa kuwa na mawazo dhahiri kabisa. Pia wanajua jinsi ya kufanya uamuzi vyema. Wana uwezo wa kufikiria kuhusu mambo yasiyo husishwa na ukweli.

Katika hatua hii, vijana kwa wakati mwingi hawakubaliani na maoni ya wazazi wao na huhusika katika mijadala ili kueleza maoni yao kwenye mjadala.

Ukuaji huu wa kimawazo utaonekana vijana hawa wanapo fanya kazi zao za ziada, kutangamana na watu na katika majukumu mengine. Hata wanapo zidi kukua kimawazo, hawawezi fanya vitu vingi peke yao. Jambo la kwanza kujua, ni kuwa katika umri huo, bado wanafanya uamuzi wa mbio na huenda ikawa kuwa maamuzi yao yana doa. Huenda wakawa bado hawana uwezo wa kufikiria kwa umakini.

Vijana wako huru

Mojawapo ya ishara muhimu za vijana ni uhuru. Vijana watakuwa na usemi mkuu katika mambo ambayo yanaendelea kwenye familia. Wanasema mawazo yao kwa mambo yote kutoka kwa chakula, nguo hadi kwa masharti ya nyumba.

Kijana wako atakuwa na tabia tofauti ikilinganishwa na alipokuwa mtoto. Ila, haupaswi kuangazia uhuru wao kana kwamba ni jambo hasi, kwa sababu wanahitaji kuishi vyema na jamii kubwa. Haitakuwa sawa kwao kutegemea wazazi maishani mwao mote.

Punde unapojua tabia za vijana, itakuwa rahisi kwako kupumzika na kufurahikia hatua hii ya maisha yao.

Kumbukumbu: NHS

BBC Science

The Healthy Place for Mental Health 

Livestrong

Soma pia: How to deal with a bully, according to my bullied 7-year-old

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio