Mambo 5 Ya Kufanya Mchumba Wako Anaposema Vitu Vya Kuumiza

Mambo 5 Ya Kufanya Mchumba Wako Anaposema Vitu Vya Kuumiza

Kuwa sawa ni fikira tu isiyo ya kweli. Haiwezekani wakati wote kufanya mambo mema ama kusema maneno mazuri. Makosa huenda yaka tendeka. Walakini, mchumba wako anapo sema vitu vya kuumiza, huenda ikawa vigumu kusahau walivyo kufanya uhisi wakati huo.

Kwa ufupi, tunatarajia kuwa wachumba wetu watakuwa makini na maneno yao. Matusi kwa mara nyingi hupuuzwa kwenye ndoa kwa sababu sio kama kuchapwa na hakuna ushahidi kuonyesha kuwa ulitusiwa. Ila, maneno mabaya yanaweza tumika kama silaha ya kusababisha uharibifu. Kusema maneno mabaya kunaweza sababisha uchungu wa hisia na kufanya wanandoa wakosane.

Iwapo haisababishi kupatiwa talaka, huenda ikasababisha tofauti kati yenu, vita na kufanya mchumba wako ahisi kana kwamba hamfaani.

Vitu 5 vya mchumba wako anapo sema vitu vya kuumiza

5 Things To Do When Your Spouse Says Hurtful Things To You.

 

Wakati ambapo mchumba wako anapo sema vitu vya kuumiza, sio mwito wa kupata talaka. Hapo awali, tulisema kuwa, kuwa sawa katika mambo yote ni fikira tu na hakuwezekani. Kwa hivyo, kutarajia kuwa mchumba wako wakati wote atasema mambo unayo tarajia, na jinsi unavyo taka yasemwe huenda ikawa haiwezekani.

Mara nyingi, tunajua kuwa mchumba wetu anatupenda kwa kweli na huenda ikawa tu alikuwa anapitia wakati mgumu. Iwapo unashangaa cha kufanya mchumba wako anaposema vitu vya kuumiza, hapa kuna vidokezo vitano:

 

1.   Wajulishe kuwa wamekuumiza

Huu sio wakati wa kumnyamazia mchumba wako. Iwapo walisema kitu ambacho kili kuumiza, lazima uwaambie ilivyo kufanya uhisi. Ukweli ni kuwa baadhi ya wakati, huenda ikawa hawa kukusudia kukufanya uhisi vibaya. Pia, mchumba wako hajui kusoma akili. Usipo waambia, huenda ikatendeka tena kwa sababu hawajui kuwa maneno yao yana kuumiza.

2.   Sema ilivyo kufanya uhisi

mchumba wako anapo sema vitu vya kuumiza

Jaribu kuwa shwari na maneno yako. Kuwajulisha kuwa hisia zako zimeumizwa ni hatua nzuri, hatua inayo fuata ni kusema jinsi ulivyo hisi. Kwa mfano, iwapo mchumba wako alikukasirikia mkiwa mahali pa umma, unaweza sema, "Uliniumiza jinsi ulivyo nikasirikia hapo awali. Ili fanya nika hisi kuto heshimiwa."

3.   Ipe wakati/ nafasi iwapo ume kasirika.

Mambo mawili yasiyo sawa haya tengenezi usawa wowote. Kwa wakati huo ambao ume umizwa, huenda ukafanya jambo ama kusema maneno yatakayo mwumiza mchumba wako. Masaa machache ya kunyamaza na kupumua huenda yaka kutuliza. Itasaidia zaidi ukiongea na mchumba wako kwa njia yenye utulivu zaidi.

4.   Uliza kwa nini walisema walicho sema

Hakuna sababu zinazo kubalika za kutumia maneno ya kuumiza ili kudhuru mwingine. Walakini, kumwuliza mchumba wako kwa nini alitumia maneno ya kuumiza kutasaidia. Nyote wawili mnaweza angazia njia bora zaidi ambazo angeweza kusema alicho taka. Cha kuongeza, huenda ukawa na sababu za tabia zako na kuelewa sababu zao.

5.   Mtembelee mshauri iwapo ni tabia yenye uzoefu

Huezi fanya kila kitu peke yako. Kuna wataalum na washauri wa ndoa na walio somea hasa kukumbana na matatizo kama haya na kuwasaidia wanandoa na mazungumzo yao na kadhalika. Unaweza chagua kwenda kwa mtu ambao nyote wawili mna heshimu ama hata mchungaji wenu. Walakini, mshauri aliye na vyeti atawasaidia kukumbana na tatizo mnalo pitia.

Ni mwito wa talaka mchumba wako anapo sema vitu vya kuumiza?

mchumba wako anapo sema vitu vya kuumiza

Kutofautiana ni maarufu sana katika ndoa. Jaribu kutatua tofauti zenu mnavyo weza. Pia, husisha wataalum iwapo inaonekana ni zaidi ya muwezavyo. Mwonyeshe mchumba wako mapenzi kwa kujaribu kuelewa sababu zake.

Soma pia: Successful marriage tips: how to build a long-lasting union

Chanzo: The Huffington Post

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio