Ishara 10 Za Mama Mkwe Mwenye Wivu Na Jinsi Ya Kutangamana Naye

Ishara 10 Za Mama Mkwe Mwenye Wivu Na Jinsi Ya Kutangamana Naye

Baadhi ya wamama walio wekeza maisha yao yote kwenye familia zao na hasa katika watoto wao wa kiume, huwa na wakati mgumu kuwa achilia. Huenda akawa alikuwa ana fanya uamuzi katika kila jambo maishani mwake, hadi alipo pata bibi. Wakati huu kwani kuna bibi kwenye picha, hayo yote yame badilika. Kuna mwanamke mwingine muhimu kwenye maisha ya kijana wake na hakupendi kwa hili. Kufanya mambo yawe mabaya zaidi, wewe ni mchanga, naye amekula chumvi kiasi. Iwapo bado hamja oana, kuna ishara za mama mkwe mwenye wivu za kuangazia.

Ishara 10 Za Mama Mkwe Mwenye Wivu Na Jinsi Ya Kutangamana Naye

Walakini, kwa wanawake wengi walio olewa, jambo hili lina shuhudiwa kila mara. Iwapo uko katika viatu hivi, mama mkwe wako wakati wote anatafuta njia za kukupuuza ili atosheleze wivu wake. Wakati ambapo mama mkwe wako hufikiria kuwa nyote wawili mnajihusisha katika vita vya mtoto wake wa kiume, huenda ukapata fikira nyingi za kihisia na kiakili.

Ishara Za Mama Mkwe Mwenye Wivu Za Kuangalia Ni Kama Zipi?

Ishara 10 Za Mama Mkwe Mwenye Wivu Na Jinsi Ya Kutangamana Naye

Una mama mkwe mwenye wivu iwapo yeye hufanya mojawapo ya vitu vifuatavyo:

  • Haheshimu mipaka yako hata baada ya kumwomba mara nyingi. Hajali kuheshimu mipaka yako ama maisha yako binafsi.
  • Ana egemea pakubwa kwa mtoto wake wa kiume kihisia. Ana jaribu kupata uangalifu mwingi kila mara na kujaribu kuonekana kuwa yeye ndiye mwathiriwa.
  • Anajaribu kumfanya mwanawe kufanya yote anayo yataka. Na pia kujaribu kufanya uamuzi katika nyumba yako.
  • Ana shindana nawe, aina hii ya mashindano sio sawa.
  • Ana jaribu kucheza mwathiriwa ili apate kusikizwa na bwanako.
  • Wakati wote kuteta kukuhusu kwa bwanako.
  • Ana kasirika, kutusi familia yako na kuongea mabaya kukuhusu.
  • Ana kupuuza katika mikutano ya familia na sherehe.

Njia Za Kukabiliana Na Mama Mkwe Mwenye Wivu

mama mkwe mwenye wivu

Ili kuwa na amani maishani, kufanya ndoa yako iwe rahisi zaidi, tuna kudokezea baadhi ya njia za kukabiliana na mama mkwe mwenye wivu. Ni matumaini yetu kuwa vidokezo hivi vitakusaidia na utaweza kuwa na uhusiano bora zaidi naye. Hakupaswi kuwa na mashindano kwenye nyumba, mbali mnapaswa kutangamana.

Elewa hisia zake

Badla ya kumkasirikia ama kuanza vita naye, unapaswa kuelewa kwanza kinacho sababisha tabia yake. Wanawake wote ni viumbe wenye hisia. Jaribu kuangalia tabia yake na vitu vinavyo mfanya kuwa na tabia fulani. Unapo muelewa, itakuwa rahisi kwako kuzungumza naye.

Msikize anacho sema

Wivu huanza kutokana na kutokuwa salama na uwoga wa mtu mwingine kuchukua nafasi yako anapo jiunga na familia yenu. Anaogopa huenda akabaki mpenzi mtazamaji kwenye maisha ya mtoto wake wa kiume. Utahitajika kuelewa kutokuwa salama kwake na kumsikiza. Kumpigia mara kwa mara kutamsaidia kujua kuwa unamfikiria. Kumtembelea mara kwa mara kutasaidia kuimarisha uhusiano wenu.

Mhusishe kwenye familia yako

mama mkwe mwenye wivu

Mwanamme uliye funga pingu za maisha naye ni ushuhuda wa ulezi mwema. Mfanye ahisi yeye ni spesheli. Mhusishe kwenye vitu vidogo. Baadhi ya wakati, mwulize akupe ushauri kuhusu ulezi na kutengeneza nyumba. Mwambie pia akupe maagizo ya kupika vyakula tofauti na huenda juhudi hizi zikakusaidia kushinda na mkasikizana.

Kubaliana na uhusiano kati yake na mvulana wake

Kitu muhimu zaidi kwa mama ni mapenzi ya mtoto wake. Wakati ambapo anajua kuwa ana mapenzi ya mtoto wake wa kiume, kukubali kutakuwa rahisi. Mwonyeshe kuwa ndoa haita ingiliana na uhusiano wake na mwanawe. Shaka zake na uwoga wake utaisha. Pia ataanza kukubali jinsi ulivyo.

Msaidie abadilike

Sio maisha yako tu ambayo inabadilika hapa. Mama mkwe wako pia anapitia mabadiliko pia. Kila kitu kwenye familia kina enda kubadilika na hajui iwapo ataweza kukumbana na mabadiliko hayo. Kama mwanamke aliye oleka hivi majuzi, kila mtu atakusikiza na kukusaidia na chochote unacho hitaji ila hakuna haja ya kuelewa kuwa mama mkwe wako pia anahitaji kufarijiwa na kuhisi salama. Ukweli huu unapuuzwa na watu wengi na ni chanzo kikuu cha kumfanya mama mkwe wako kuwa na wivu.

Unahitaji kumsaidia kutoka mwanzoni ili asione kana kwamba wewe ni tishio kwake, ila anafaa kukuona kama rafiki wake.

Mnunulie zawadi

mama mkwe mwenye wivu

Uliza bwanako ama baba mkwe wako kuhusu vitu ambavyo mama mkwe wako anapenda ama hapendi. Mnunulie zawadi za kumfurahisha. Moyo wake utaanza kugombana na akili yake. Ataona upande wako ambao hakutarajia na ata kukaribisha kwa mikono wazi.

Kumbuka kuwa mazungumzo ndiyo mizizi bora

Iwapo huwezi amini tabia ya mama mkwe wako, ongea kuihusu. Kuwa na mazungumzo ya kina. Kuwa na heshima ili asikuongeleshe kwa chuki. Mwulize kwa nini anafanya mambo anayo yafanya na iwapo kuna kasoro yoyote. Huenda ukashtuka kwa jinsi ambayo mazungumzo mafupi huenda yakafanya mambo yawe rahisi. Huenda ukagundua kuwa wawili wenu hamkuwa mnaelewana!

Epuka vita

Ili kudumisha amani kwenye nyumba hiyo, ni vyema kuepuka vita na mijadala ambayo huenda ikazua vita. Vita vitafanya hali hii iwe mbaya zaidi na kusababisha chuki kwenye familia. Vita fanya wanajamii wengine waanze kuchagua pande na sio jambo la busara. Ndoa yako ndiyo itakuwa uhusiano utakao athirika zaidi na haya yote.

Ongea na bwanako

mama mkwe mwenye wivu

Kuwa na mazungumzo na mume wako kuhusu tabia za mama mkwe wako huenda yaka saidia. Usitete kumhusu kwa bwana yako. Mwambie baadhi ya vitu ambazo huenda zikawa zinakusumbua. Mwulize aongee na mamake na kujua chanzo cha tabia ile kwa njia isiyo na makali. Huenda kijana wake akaweza kumfikia mamake vyema zaidi kukuliko na kumaliza vita kati yenu.

 

Soma pia: “I thought motherhood would be a mix of ice-cream and dodo

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio