Jinsi Ya Kumnasa Mwanamme Ni Kwa Kupitia Tumbo Yake Ama La?

Jinsi Ya Kumnasa Mwanamme Ni Kwa Kupitia Tumbo Yake Ama La?

Siku za hapo awali, wazazi wange hakikisha kuwa binti zao walijua jinsi ya kupikia. Sababu haikuwa kwa sababu mabinti hawa walihitaji kujua jinsi ya kujilisha. Ilikuwa zaidi ya hilo. Imani maarufu ni kuwa hiyo ilikuwa jinsi ya kumdata mwanamme, na kwa hivyo mwanamme huyu alipaswa kuwa bora zaidi kwa mapishi. Kuwa, jinsi ya kumnasa mwanamme ni kwa kupitia tumbo yake, kama walivyo sema.

jinsi ya kumnasa mwanamme

Je, Jinsi ya kumnasa mwanamme ni kwa kupitia tumbo yake?

Watu duniani kote wanapenda chakula kizuri, ila kuwa na uwezo wa kupika vyema jikoni sio dhamana kuwa mwanamme atakupenda. Mwanamke mmoja alimwambia bintiye kuwa asijue kupika tu, ila pia kujua mapishi zaidi ya mwanamke yeyote aliye maishani mwa mwanamme wake. Mashindano ya upishi yalikuwa mbinu ya mwanamke huyo. “Iwapo mapishi yako ni bora, mwanamme wakati wote atakuchagua mbadala ya mpishi ovyo,” alisema.

Bintiye alijitahidi na kujua jinsi ya kupika vyakula tofauti na kuwa mpishi bora zaidi. Ila, hata na uwezo huu wa sekta ya jikoni, mumewe alichagua mtu mwingine. Na kumthibitishia kuwa, usemi “jinsi ya kumnasa mwanamme ni kwa kupitia tumbo yake,” ni imani isiyo ya kweli.

Kama kupika sio njia ya kumnasa mwanamme, utampataje mwanamme na kuhakikisha kuwa anakupenda?

Mwaname mzee mara moja alisema kuwa njia ya kumnasa mwanamme sio kwa kupitia kwa tumbo yake. Ushauri wake ni kuwa wanawake wanao taka kuwa data wanaume wanapaswa kuwa makini na sehemu chini ya mshipi. Kufunga jicho moja kwa mzaha kuliko fuatia ushauri wake ni kuwa hakuamini kuwa mwanamme hangekupenda kwa sababu ya kufanya mapenzi.

jinsi ya kumpata mwanamme

Kupika ni jambo la lazima na kila mtu lazima ajue jinsi ya kupika

Kwa nini unapaswa kutupilia mbali imani kuwa kumpikia mwanamme kutamnasa

1. Chakula kizuri kiko kila mahali

Kupika ni muhimu ili uishi, na kuna nafasi kubwa kuwa mchumba wako anajua jinsi ya kujipikia. Wapishi wa kiume wanaitawala tasnia ya vyakula. Hata kama hawezi, anaweza pata aina zote za vyakula vyenye ladha. Ukitembelea hoteli, utagundua kuwa idadi kubwa ya wateja huko ni wanaume, na wengi wao wameoana, ila wanapenda kula nje ama kwenye mahoteli hata kama bibi zao wanaweza kuwapikia chakula kitamu.

2. Chakula kizuri sio mbadala wa tabia zisizo pendeza

Kuna maana gani kusema kuwa njia ya kumnasa mwanamme ni kwa kupitia tumbo yake wakati ambapo anafika nyumbani kukusumbua na kuanza vita? Badala ya kusoma njia tofauti za kutayarisha chakula, anza kuwa mke ambaye bwanako angependa kuja nyumbani kwake. Hatua ya kwanza ni kuwacha tabia zote hasi na kutia bidii kuwa mke mwema.

3. Upishi mwema sio muhimu vile iwapo uhusiano wenu hauandamani vyema

Haijalishi kiasi ambacho wali ama sima yako ni tamu na ya kupendeza, uhusiano ambao hauna utangamano haujalishi iwapo upishi wako ni wa kiwango cha kitaifa. Lishe zako zitakupa mwanamme ambaye hufurahia lishe zilizo pikwa nyumbani. Ila chakula chako hakitamfanya akupende. Utavunjika moyo iwapo umeishi kuamini kuwa njia ya kumnasa mwanamme ni kupitia kwa tumbo.

Kupika ni jambo muhimu kwa kila mtu- wake kwa waume wote-  wanapaswa kujua jinsi ya kujilisha. Kutarajia mtu akupende kwa sababu ya chakula kutakuvunja moyo. Ukimpata mtu anaye kufaa, mapishi mema yatakuwa jambo la ziada.

Soma pia: Ofada rice recipe

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio